from
left to Right – Sangita Reddy, Chairperson, Apollo Sugar and Joint
Managing Director, Apollo Hospitals, Christopher A. Viehbacher, Chief
Executive Officer, Sanofi, Dr. Prathap Reddy, Chairman – Apollo
Hospitals Group and Dr. Deepak Chopra, Renowned Global Spiritual Guru.
Hospitali
maarufu za kimataifa za Apollo ambazo zimeazimia kufungua hospitali na
kliniki mbali mbali nchini, hivi karibuni zimetangaza uamuazi wake wa
kushirikiana na Sanofi katika upanuzi wa Kliniki za Kisukari za Apollo
ambazo zinatatoa huduma jumuishi kwa wagonjwa wa kisukari nchini India.
Watanzania wanatazamia kufaidika kutokana na uhusiano uliopo kati ya
nchi ya Tanzania na hospitali za Apollo kwahuduma zinazotolewa kwa
wagonjwa wanaoenda kupata matibabu nchini India.
Kupitia
uhusianoi huo, Apollo na Sanofi wameratibu kutumia ujuzi walionao
kwenye masuala ya ugonjwa wa kisukari kutoa huduma bora kupitia elimu,
matibabu na mipango itakayosaidia wagonjwa wa kisukari kupata ahueni.
Hatua ya kwanza ya uhusiano imelenga kuanzisha kliniki za kisukari
hamsini (50) kote nchini India.
Magonjwa
yasiyoambukizwa hupelekea vifo vya watu milioni 36 kila mwaka ambvyo ni
sawa asilimia 80% vingi vikirekodiwa katika nchi zenye vipato vya chini
na kati. Zaidi ya hayo, mzigo wa kiuchumi nchini Tanzania
unaosababishwa na hasara itokanayo na magonjwa ya kisukari na moyo
inafikiriwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa zaidi ya bilioni 2.5
za dola za Kimarekani kati ya 2005 na 2015. Nchini Tanzania, magonjwa
yasiyoambukizwa hupelekea asilimia 31% ya vifo vya watu kulingana na
takwimu zilizotelewa na shirika la Afya Duniani (WHO) kwenye takwimu za
nchi mbali mbali duniani.
Shirikisho
la Kimataifa la Kisukari (IDF) linakadiria watu milioni 382 duniani
walio na ugonjwa wa kisukari ikiwa zaidi ya watu milioni 19 kutoka bara
la Afrika wakati kesi za takriban watu 1,706,930 wenye kisukari
zimeripotiwa mwaka 2013.
from
left to Right – Sangita Reddy, Chairperson, Apollo Sugar and Joint
Managing Director, Apollo Hospitals, Christopher A. Viehbacher, Chief
Executive Officer, Sanofi, Dr. Prathap Reddy, Chairman – Apollo
Hospitals Group, Dr. Deepak Chopra, Renowned Global Spiritual Guru and
Gagan Bhalla, CEO, Apollo Sugar.
Katika
jitihada za kudhibiti ushamiri wa janga la kisukari duniani, Kliniki za
Kisukari za Apollozimelenga kuondoa maradhi yatokanayo na ugonjwa wa
kisukari kwa kutoa huduma rahisi na bora ndani ya kliniki itakayopelekea
ugunduzi wa mapema na tiba mbadala kwa wagonjwa wa kisukari na matatizo
yatokanayo na ugonjwa huo, na mfumo bora wa maisha na mabadiliko ya
tabia.
Akizungumzia
uhusiano huo, Dkt. Dr. Prathap Reddy, Mwenyekiti – Apollo Hospitals
Group shared, “Kwa muda mrefu, Hospitali za Apollo zimeongoza duniani
katika kutoa huduma bora za afya kulingana na viwango na taratibu za
huduma za afya. Na ongezeko la ugonjwa wa kisukari, jamii inabidi
kufanya maamuzi haraka yenye nia kutokomeza ugonjwa huu unaosababisha
vifo vya watu wengi. Ni Imani kwamba kupitia Kliniki za Apollo
tutafanikiwaw to kuwapa wagonjwa wa kisukari huduma za kisasa na ushauri
ambao utawasaidia kuangalia afya zao. Huu ni mwanzo mzuri katika
kuboresha miundo mbinu ya kutibu kisukari. Ndoto yetu ya pamoja
itasaidia kufanya njia mpya za kuhudumi wagonjwa wa kisukari ambayo
inatafaidisha wagonjwa hao.”
“Sanofi
ina takriban miaka 100 ya urithi katika masuala ya kuendeleza matibabu
ya kisukari na inafahamu shinikizo walilonao wataalamu kwa wagonjwa
wanaoangalia afya zao za kisukari alisema Christopher A. Viehbacher,
Afisa Mkuu Mtendaji, Sanofi.” Kwa kuungana pamoja na kuanzisha Kliniki
za Kisukari, Sanofi na Apollo wanaonyesha jitihada zake kwa wagonjwa wa
kisukari zinazotoa mchango kwa kila hatua ya ugonjwa wa kisukari ili
kupunguza mzigo.
Huku
kukiwa na ongezeko la watu wanaougua kisukari duniani, wagonjwa wengi
bado hawatambui hali zao za kiafya ama kutoangalia hali zao vizuri.
Wagonjwa hawa wanahitaji uelewa kuhusu ugonjwa huu na kupata huduma za
kisasa. Katika mawazo haya,Sangita Reddy, Mwenyekiti, Apollo Sugar na
Mkurugenzi Mtendaji, Hospitali za Apollo, alisema “Apollo imetambuliwa
na American Diabetes Association kwa utoaji wa huduma wenye mafanikio
kwa wagonjwa wa kisukari kwa mara ya kwanza nchini India. Lakini, kama
taifa bado tunapambana kutambuliwa kama senta ya kisukari duniani.
Tunatambua kuwa kugundulika na ungonjwa wa kisukari na kulazimika
kubadili mwenendo wa maisha huogopesha wagonjwa, hivyo, tumedhamiria
kuwasaidia wangonjwa kupata ushauri na matibabu sahihi. Katika kliniki
hizi wagonjwa wa kisukari wataweza kujipatia habari, ushauri na matibabu
na uangalizi. Tumedhiria kupeleka huduma sehemu nyingi.”
Kliniki
ya Sukari ya Apollo ni sehemu ya tawi la Apollo Health & Lifestyle
ambalo linachangia kwa kasi katika ukuaji wa afya. Kama ilivyo kwa
wagonjwa wa kusikuri nchini India, hali kadhalika kwa wangonjwa wa
kisukari nchini Tanzania hutumia pesa nyingi kwa mwaka kupata matibabu
ikiwa ni kiasi cha dola za kimarekani $31 wakati hatua za mwisho za
ugonjwa hugharimu mara 10 hadi 18 zaidi. Gagan Bhalla, Afisa Mkuu
Mtendaji, Apollo Sugar alimalizia kwa kusema, “Aina hii ya gharama
inaweza kusababisha athari kubwa za kiuchumi kwa familia na hata
kupelekea madeni. Katika kliniki yetu tunaamini kuwa kwa huduma bora na
kisasa, na uangalizi wa karibu wa mienendo kwa wa wagonjwa wa kisukari
italeta matokeo mazuri.
0 comments:
Post a Comment